Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai, 2017
Picha
Katibu Mkuu Wizara Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Nd Juma Ali  Juma akitoa ufafanuzi juu ya fursa za uwekezaji katika sekta ya kilimo mbele ya ujumbe wa w awekejaji  kutoka Malaysia waliofika ofisi za kilimo huko Maruubi. ( Kulia kwake ni Waziri wa Kilimo na Wakurugenzi wa Wizara ya Kilimo ).
Picha
NZI WAHARIBIFU WA MATUNDA. UTANGULIZI Zanzibar ni sehemu ambayo wananchi wake wanategemea zaidi Kilimo cha mazao mbali mbali ikiwemo uzalishaji wa matunda na mbogamboga kwa ajili ya chakula pamoja na  biashara kwa kipindi kirefu. Wananchi wakijipatia kipato kwa kukidhi mahitaji na maisha yao ya kila siku pamoja na kunyanyua uchumi wa nchi mazao kama Embe ya Borobo Muyuni zilikua zikisafirishwa hadi nchi za Kiarabu na Ncui kuingiza pesa za kigeni, lakini miaka ya karibuni pamejitokeza wadudu wapya  waharibifu  wa matunda ambao wamesababisha kiwango cha uzalishaji wa mazao hayo kupungua hali iliyosababisha kukosekana kwa soko la ndani na la nje ya nchi kwa ajili ya usafirishaji wa matunda  na kuweza kukosesha Zanzibar Fedha za kigeni kupitia uzalishaji wa matunda. ASILI YA NZI WAGHARIBIFU WA MATUNDA. Nzi wagharibifu wa Matunda wameenea karibu ulimenguni kote isipokua katika Bra la Antaktika, Nzi hao wamegawanyika katika jamii mbali mbali , kati ...
Picha
Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mh. Hamad Rashid Mohamed akimsikiliza Balozi wa Tanzania Nchini China Mh. Mbelwa Kairuki aliekuja kumtembelea Ofisini kwake  Maruhubi.
Picha
Maafisa wa Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) wakishiriki zoezi la uvunaji wa mpunga kwenye  shamba darasa lililotoa mafunzo  ya ukulima kwa kutumia mbinu mpya ya ukulima wa mpunga itwayo  kilimo shadidi, mafunzo yalitolewa na Mradi wa kuongeza Uzalishaji na Tija katika Zao la Mpunga, uvunaji huu umefanyika huko kwenye Kambi ya Upenja Mkoa wa Kaskazini.  
Picha
MPANGO KAZI WA UZALISHAJI WA ALIZET
Picha
WAZIRI WA KILIMO, MALIASILI, MIFUGO NA UVUVI AZINDUA BODI TATU-July 2017 Waziri wa kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Mhe. Hamad Rashid Mohamed amesema madhumuni ya kuazishwa kwa bodi ya kampuni ya uvuvi ya Zanzibar (ZAFICO) ni kuimarisha miundombinu na kuendeleza Uvuvi kibiashara, pamoja na kuazisha viwanda vya samaki nchini. Uwepo wa kampuni kutaongeza upatikanaji wa ajira kwa vijana na kukuza kipato cha wananchi na kuwawezesha wavuvi wadogo wadogo kuvua katika bahari ya kina kirefu. Hayo aliyaeleza wakati akizinduwa bodi ya Mamlaka ya Uvuvi, na kuchaguliwa kwa ndugu Omar Hassan Omar kuwa Mwenyekiti wa bodi hiyo. Wakati huo huo Mhe. Hamad alizinduwa Bodi ya wakurugenzi taasisi ya utafiti wa Mifugo na kuitaka bodi kufanya tafiti kwa kutumia teknologia za kisasa ili kuweza kupata taarifa kamili za wafugaji, ardhi, maji na maeneo ya kufungia kwani hii itapelekea thamani ya nyama na kututoa kwenye ufugaji duni ambao hauleti tija kwa wafugaji walio wengi. Pia Mhe. Hamad amesisi...
Picha
Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mh. Hamad Rashid Mohamed akiwa na balozi mdogo wa China nchini Tanzania Nd. Xie xiaowu pamoja na washiriki wa mafunzo ya ufugaji wa mazao ya baharini huko Maruhubi
Picha
Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mh. Hamad Rashid Mohamed amekutana na Naibu mwakilishi wakudumu kutoka Israel Nd Michael Baror ofisini kwake Maruhubi.
Picha
BODI YA USHAURI YA WAKALA WA SEREKALI WA HUDUMA ZA MATREKTA NA ZANA ZA KILIMO Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mh. Hamad Rashid Mohamed akiwa katika picha ya pamoja baada ya kuidhindua Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Serekali wa Huduma za Matrekta na Zana za Kilimo
Picha
Waziri wa Kilimo,Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mh. Hamad Rashid Mohamed akipata maelezo kutoka kwa mkulima anaetumia mbinu mpya ya ukulima wa kilimo shadidi  huko bonde la Chehu
Picha
Athari za uchimbaji mchanga kiholela ulivyoathiri maeneo ya kilimo
Picha
Shamba darasa la mpunga lililopo JKU Upenja linalofundisha ukulima wa mpunga kwa kutumia mbinu mpya ya kilimo cha mpunga itwayo kilimo shadidi. Muonekano wa shamba darasa lililopandwa kwa mbinu mpya ya kilimo shadidi Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi akikagua Shamba darasa la mpunga lililopanda kwa kutumia mbinu mpya ya kilimo shadidi
Picha
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi akishiriki zoezi la uvunaji wa mpunga, kwenye  mpango wa  majaribio wa heka hamsini  kwa  kila wilaya    kuwapa wakulima pembejeo zote za kilimo, uvunaji huo umefanyika kwenye bonde la Pangeni mkoa wa Kaskazini Unguja