NZI
WAHARIBIFU WA MATUNDA.
UTANGULIZI
Zanzibar ni sehemu
ambayo wananchi wake wanategemea zaidi Kilimo cha mazao mbali mbali ikiwemo
uzalishaji wa matunda na mbogamboga kwa ajili ya chakula pamoja na biashara kwa kipindi kirefu. Wananchi wakijipatia
kipato kwa kukidhi mahitaji na maisha yao ya kila siku pamoja na kunyanyua
uchumi wa nchi mazao kama Embe ya Borobo Muyuni zilikua zikisafirishwa hadi
nchi za Kiarabu na Ncui kuingiza pesa za kigeni, lakini miaka ya karibuni
pamejitokeza wadudu wapya waharibifu
wa matunda ambao wamesababisha kiwango cha uzalishaji wa mazao hayo
kupungua hali iliyosababisha kukosekana kwa soko la ndani na la nje ya nchi kwa
ajili ya usafirishaji wa matunda na
kuweza kukosesha Zanzibar Fedha za kigeni kupitia uzalishaji wa matunda.
ASILI
YA NZI WAGHARIBIFU WA MATUNDA.
Nzi wagharibifu wa
Matunda wameenea karibu ulimenguni kote isipokua katika Bra la Antaktika, Nzi
hao wamegawanyika katika jamii mbali mbali , kati ya jamii hizo ni jamii sita
zinazofanya uharibifu wa matunda na mboga mboga. Katika jamii hizi kuna aina
mbali mbali za nzi wagharibifu. Hata hivyo kila jamii ina asili ya eneo au
maeneo Fulani ya Kijografi . Jamii zenye asili ya bara la Afrika ni Dacus na
Ceratitis . Zipo baadhi ya aina za Nzi wagharibifu wa matunda ambazo zimevamia
maeneo mengine kwa mfano Nzi wa Mediterenian (Ceratitis Capitata) ni Nzi mwenye
asili ya Afrika , lakini kwa sasa amesambaa karibu ulimwengu wote, vile vile
Nzi mvamizi (Bactocera Invadens ) mwenye asili ya Bara la Asia amevamia Bara la
Africa mwaka 2003. Nzi wagharibifu wa Matunda ni tofauti na wale Nzi wadogo
wanaojulikana kwa jina la Drosophila ambao huonekana kwenye matunda na vyakula
vilivyooza.
Katika Visiwa vyetu kuna
Nzi tofauti waharibifu wa Matunda wenye asili ya Afrika na Yule wavamizi kutoka
Bara la Asia, wale wenye asili ya Afrika mashambulizi yao ni madogo kutokana na
uwezo wao mdogo wa kuzaliana vile vile kuwepo kwa maadui zao, na walikua
wakisababisha hasara kati ya asilimia 20% na 30%.
Nzi Mvamizi mwenye Asili
ya Bara la Asia anasababisha hasara kubwa hadi asilimia 90% kutokana kuzaliana
kwa wingi, na kula aina nyingi za Matunda pia kutokua na madui kwa kua yeye ni
mgeni katika Bara letu. Kwa sasa Nzi mvamizi amesambaa katika visiwa vyetu vya
Unguja na Pemba hali iliopelekea wadudu wenye asili ya bara la Afrika kuonekana
katika maeneo machache na kwa idadi ndogo sana.
Leo tunamzungumzia Nzi
mvamizi (Bactocera Invadens ) Jinsi ya muonekano wake, Uzazi wake, Athari
zake na Jinsi ya kumzibiti.
KUTAMTAMBUA
NZI MUHARIBIFU WA MATUNDA
Nzi
mharibifu anonekana ni sawa na nzi wa nyumbani lakini yeye ana umbo la
manyigu/Uvi ana rangi ya udongo inayong’aa,ana alama ya T mgongoni,ana rangi ya
Dhahabu pia ana rangi ya manjano kifuani na miguuni. Nzi huyu anapatikana
katika mazingira tofauti kama vile mashambani, masokoni, majumbani na maeneo
yote ambayo yanapatikana matunda na mboga mboga.
Nzi huyu anashambulia zaidi
ya aina 40 za matuda kama vile Mapera, papai, Embe mtofaa, doriani, machungwa, mapea,
karambola, tikiti, matango, maboga, Zukini, embe sakua, kungu, chongoma, kunazi
na mengineo.
Nzi huyu huyashambulia
matunda katika hatua zote za ukuaji wa matunda husika,yaani Matunda yanapokua
machanga ,mapevu na yanapokua mabivu.Hushambuliwa yakiwa kwenye mti,yakiwa
chini ya mti yanapokua yamehifadhiwa nyumbani na hata yakiwa sokoni.
MAISHA
YA NZI MUHARIBIFU WA MATUNDA
Nzi jike mara baada ya
kukutana na nzi dume hutaga mayai yake ndani ya tunda milimeter 2-3 kwa kutumia
mwiba wake uliko mkiani (Ovipositor).Na mayai hayo hutagwa kwa vichungu
vichungu,3 hadi 8 hutegemea na aina nzi mwenyewe na nzi huyo ana uwezo wa
kutaga mayai yasiopungua 1500 kilingana na hali ya hewa na upatikanaji wa
chakula.
Mayai meupe yenye
umbile la ndizi huanguliwa kua funza baada ya siku 3 hadi 12 kulingana na hali
ya hewa.
Funza huendelea kukua
ndani tunda kwa kula nyama ya tunda hilo na kusababisha uharibifu. Funza akiwa
ndani ya tunda hubadilisha ngozi yake mara mbili katika hatua zake za ukuaji .
Kwa hatua hii ya ukuaji
wa funza,tunda hilo huoza na mara nyingi huanguka chini na funza hutoka ndani
ya tunda na kujifukia katika udongo 2cm hadi 5cm ili kupitia hatua yake
nyengine ya ukuaji ya Buu/pupa. Pupa lina rangi nyeupe,rangi ya udongo au
nyeusi
Pupa hukaa siku 10 hadi
20 kwenye udongo ili aweze kutoka tena baadae na kugeuga nzi kamili inategemea
na hali ya hewa.
DALILI
ZA MATUNDA YALIOSHAMBULIWA
Matunda yalioshambuliwa
yanatofautiana kati ya tunda na tunda. kwa upande wa nje ya tunda utaweza kuona
mabaka (jamii ya baka la uozo).
Kwa dalili zandani
utaona mafunza kwenye nyama ya tunda lililooza. Fenesi na Doriani endapo itakua
yamepasuka pia hushambuliwa na Nzi mugharibifu watunda. Baaddhi ya matunda huwa
hayashambuliwi na Nzi mpaka yawe yamepea sana au kuiva kwa mfano Papai na ndizi
.
NJIA
ZA KUMDHIBITI NZI MUHARIBIFU WA MATUNDA.
Nzi muharibifu wa
matunda wanaweza kudhubitiwa kwa kutumia mbinu mchanganyiko (IPM) Mbinu
mchanganyiko ni mpango unaochanganya mbinu mbali mbali kwa wakati mmoja, lengo
kuu likiwa ni kupunguza matumizi ya madawa na hatimae kutunza mazingira,kulinda
afya ya mlaji na kupunguza gharama za uzalishaji. Miongoni mwa mbinu Mchanganyiko
za kuwadhibiti Nzi waharibifu wa matunda ni kuzuia kuingia kwa Nzi wageni
(KARANTINI), usafi wa shamba, kuangamiza madume, kutumia wadudu rafiki, kufunga
matunda kwa mifuko, matumizi sahihi ya madawa na kuvuna mapema,
Njia zote hizo endapo
zitatekelezwa kwa ufanisi kwa pamoja zinaweza kupunguza kiasi kikubwa tatizo la
nzi wagharibifu wa matunda
UFAFANUZI
WA NJIA ZA KUMDHIBITI NZI.
1. USAFI WA SHAMBA
·
Palilia eneo la mti linalolingana na
mwamvuli wa matawi yake
·
Fyeka sehemu nyengine za shamba
zisizokua na miti ya matunda ili kuhifadhi wadudu rafiki,kutunza unyevu na
kuzuia mmong’onyoko wa udongo.
·
Punguza/Pogoa matawi kwa kuzingatia
maelekezo ya wataalamu
·
Okota matunda yote yaliodondoka na
kuyafukia kiasi cha mita moja ardhini, au kuyaweka katika mifuko meusi ya
plastic na kuyaanika juani, kulisha mifugo, kuyazamisha kwenyemaji kwa siku
tatu na kutengeneza mbolea ya mboji. Pia Matunda yanaweza kuwekwa ndani ya hema
la chandarua la kutunzia wadudu rafiki
2. KUDHIBITI KUINGIA KWA NZI WAGENI
(KARANTI)
·
Kuweka mitego yenye dawa za kuvutia
wadudu katika mashamba ya Mipaka ya Nchi, Bandari na Viwanda vya Ndege na
Masoko ili kutambua uwepo wa nzi wageni.
·
Kukagua matunda yanayoingizwa Nchini kwa
kuchunguza dalili za uharibifu kama vile kitobo,kuoza, kuiva upande na ikibidi
tunda likatwe na kuchunguzwa kuepo kwa mafunza.
·
Kuzuia kuingia kwa matunda Nchini endapo
yameshambuliwa na Nzi wagharibifu wa Matunda.
·
Kuhakikisha Mwananchi unakua na kibali
cha kusafirishia mazao kwa ajili ya kutolea bidhaa za kilimo nje ya nchi
(Phytosanitary Certificate) na kwa
anaengiza ndani ya nhi awe na kibali cha (Importation Permit ).
·
Toa taarifa kwa vyombo husika juu ya
kuwepo kwa matunda yalioshambuliwa na Nzi wageni kwa hatua zaidi
3. KUTUMIA WADUDU MARAFIKI
Wadudu marafiki
wanaweza kutumika kupunguza mashambulizi ya Nzi wagharibifu wa matunda. Wadudu
kama Manyigu na Majimoto kwa kuzibiti Nzi wagharibifu wa matunda. Wadudu hawa
huwala wadudu wengine hivyo hupunguza wingi wao, nyigu hutaga mayai yake ndani
ya mdudu na hatimae humuua
Kuepo kwa majimoto
humfanya Nzi jike mugharibifu wa matunda ashindwe kutaga mayai. Majimoto pia
anaweza kula Nzi hao au kuwafukuza, ili majimoto wawe na uwezo wa kuwadhibiti
Nzi wagharibifu wa Matunda ni lazima wawe wengi shambani. Hata hivyo wingi wa
Majimoto hupungua kutokana matumizi ya madawa ya mimea , mvua kubwa, kushambuliwa
na sisimizi adui na kupungua kwa chakula ( Kama asali ya mimea na Nekta). Walishe
majimoto angalau mara moja kwa mwezi baada ya msimu wa matunda, majimoto
wanapenda vyakula vyenye Protin kama Mabaki ya Samaki na Sukari .
Tunaweza kuwalinda na
kuwastawisha wadudu rafiki ndani ya shamba la matunda kwa kuzingatia matumizi
sahihi ya madawa ya mimea, kudhibiti sisimizi kwa kuweka Urimbo kuzunguka
sehemu ya chini ya shina la mmea, kupalilia na kutengeneza kisahani kuzunguka
shina la mmea, kuepuka kuota magugu ambayo sisimizi ataweza kutumia kama daraja
la kupandia kwenye mti.
4. NJIA YA KUANGAMIZA MADUME KWA
KUTUMIA MITEGO.
Njia
ya kutumia mitego ya kuwanasia nzi, mitego ambayo ni mchanganyiko wa dawa za
aina mbili :-
Aina
ya kwanza ni ile ya kuweza kuawavutia nzi hao(methyl eugenol) ambayo inatoa
harufu inamvutia nzi dume tu, harufu hiyo humvuta nzi dume katika mtego akihisi
kama kuna nzi jike aliyeshurufu,matokeo yake anapoinga ndani ya mtego hukutana
na dawa ya pili au sumu nyengine ambayo ndio itakayomuua nayo ni (DDVP) ambayo
tunachanganya na kutumbukiza katika mtego na baadae kuwapatia wakulima na
kupeleka katika mashamba yao tayari kwa kufanya kazi ya kunasia nzi wa matunda.
Dawa
iliyomo katika mtego huo inaweza kuvuta nzi kwa masafa ya umbali wa mita 100
kila upande. Dawa hiyo ina uwezo wa kufanya kazi kwa muda wa wiki 3 hadi 4 na
nguvu ya dawa huanza hupungua uwezo wa kufanya kazi katika mtego.Hivyo wakulima
hupatiwa taaraifa za kuileta tena mitego yao kupia vituo tulivyokubaliana kwa
ajili ya kuirejeshea tena nguvu ya dawa kwenye mitego hiyo,na zoezi hilo
linatakiwa liwe endelevu.
5. KUTENGENEZA MTEGO WA KUNASIA NZI WA MATUNDA.
·
Kuandaa kikopo safi cha plastic au Chupa ya maji ya kunywa
angalau yenye ujazo wa lita moja.
·
Kutoboa madirisha 2 hadi 4 katika kikopo
hicho sehemu ambazo watapitia nzi.
·
Kutoboa mfuniko wa kikopo hicho tundu 1 kwa
ajili ya kupitishia waya wenye pamba.
·
Kuandaa pamba katika umbile la
mviringo kiasi kidogo na kuifunga waya.
·
Kuifunga pamba hiyo kwa kutumia waya
wenye urefu usiopungua futi moja.
·
Kuupitisha waya huo tuliofunga na pamba
katikati ya mfunikio wa kikopo ambacho ndo mtego wetu.
JINSI
MTEGO WA NZI UNAVYOFANYA KAZI
·
Tunachanganya dawa ya kuvutia Nzi (aina
ya methyl eugenol ) pamoja na dawa ya kuulia Nzi ( dawa aina ya DDVP ) katika
Geloni moja .
·
Baada ya hapo tunauchovya mtego wetu
kwenye dawa tulioichanganya. Mara baada ya kumaliza hatua hizo mtego utakua
umekamilika na tayari kwa ajili ya kuupeleka shambani.
·
Hakikisha mitego imeenea eneo vizuri
shambani na jitahidi sana kuilinda na jua kali.
·
Dawa hiyo ina uwezo wa kuvuta wadudu kwa umbali/masafa ya mita 50. Kutoka kila
upande wa mtego. Hivyo kila baada ya mita100 uwepo mtego mwengine
·
Dawa iliyomo katika mtego huo inaweza
kuvuta nzi kwa masafa ya umbali wa mita50-100 kila upande kwa ajili ya
kuangamiza nzi watakaoingia katika mtego huo.
·
Dawa hiyo ina uwezo wa kufanya kazi kwa
muda wa mwezi mmoja hadi mmja na nusu.
·
Kagua mtego kila baada ya siku 7, watoe
Nzi waliokufa na uwafukie .
·
Baada ya hapo kila inapotimia mwezi
mmoja na nusu Mkulima atafuata utaratibu uliopangwa kwa kufata Kituo kilicho
karibu na yeye vijijini mwao kwa ajili ya ubadilishaji dawa .
·
Pia huduma hizo za ubadilishwaji wa dawa
katika mitego zinatolewa katika vituo vya Utibabu wa Mimea Mwanakwerekwe na
Kituo cha Kilimo Kizimbani.
TAHADHARI
Njia ya kutumia
pekeyake sio njia pekee ya kumdhibit Nzi wa matunda na haipaswi itumike peke
yake ndio maana tunasisiza tutumie njia mchanganyiko (IPM) ambazo tumezieleza
mwanzoni.
WITO
KWA WAKULIMA
Tunawashauri wakulima
wote wamfahamu nzi wa matunda kua ni adui wa uchumi wetu, hivyo kwa pamoja
tushirikiane kutumia njia mbali mbali za kuwadhibiti nzi hao. ikitokea mkulima mmoja kutowajibika na
taratibu za kumdhiiti nzi huyo katika shamba lake atasababisha madhara katika
mashamba ya majirani zake. HIVYO SOTE
TUWAJIBIKE KUMTOKOMEZA NZI MUHARIBIFU WA MATUNDA.
Maoni
Chapisha Maoni