Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mh. Hamad Rashid Mohamed amekutana na Naibu mwakilishi wakudumu kutoka Israel Nd Michael Baror ofisini kwake Maruhubi.
NZI WAHARIBIFU WA MATUNDA. UTANGULIZI Zanzibar ni sehemu ambayo wananchi wake wanategemea zaidi Kilimo cha mazao mbali mbali ikiwemo uzalishaji wa matunda na mbogamboga kwa ajili ya chakula pamoja na biashara kwa kipindi kirefu. Wananchi wakijipatia kipato kwa kukidhi mahitaji na maisha yao ya kila siku pamoja na kunyanyua uchumi wa nchi mazao kama Embe ya Borobo Muyuni zilikua zikisafirishwa hadi nchi za Kiarabu na Ncui kuingiza pesa za kigeni, lakini miaka ya karibuni pamejitokeza wadudu wapya waharibifu wa matunda ambao wamesababisha kiwango cha uzalishaji wa mazao hayo kupungua hali iliyosababisha kukosekana kwa soko la ndani na la nje ya nchi kwa ajili ya usafirishaji wa matunda na kuweza kukosesha Zanzibar Fedha za kigeni kupitia uzalishaji wa matunda. ASILI YA NZI WAGHARIBIFU WA MATUNDA. Nzi wagharibifu wa Matunda wameenea karibu ulimenguni kote isipokua katika Bra la Antaktika, Nzi hao wamegawanyika katika jamii mbali mbali , kati ...
Maoni
Chapisha Maoni