NZI WAHARIBIFU WA MATUNDA. UTANGULIZI Zanzibar ni sehemu ambayo wananchi wake wanategemea zaidi Kilimo cha mazao mbali mbali ikiwemo uzalishaji wa matunda na mbogamboga kwa ajili ya chakula pamoja na biashara kwa kipindi kirefu. Wananchi wakijipatia kipato kwa kukidhi mahitaji na maisha yao ya kila siku pamoja na kunyanyua uchumi wa nchi mazao kama Embe ya Borobo Muyuni zilikua zikisafirishwa hadi nchi za Kiarabu na Ncui kuingiza pesa za kigeni, lakini miaka ya karibuni pamejitokeza wadudu wapya waharibifu wa matunda ambao wamesababisha kiwango cha uzalishaji wa mazao hayo kupungua hali iliyosababisha kukosekana kwa soko la ndani na la nje ya nchi kwa ajili ya usafirishaji wa matunda na kuweza kukosesha Zanzibar Fedha za kigeni kupitia uzalishaji wa matunda. ASILI YA NZI WAGHARIBIFU WA MATUNDA. Nzi wagharibifu wa Matunda wameenea karibu ulimenguni kote isipokua katika Bra la Antaktika, Nzi hao wamegawanyika katika jamii mbali mbali , kati ...
Machapisho maarufu kutoka blogu hii
MAKALA YA PWEZA . Fahamu maisha ya Pweza jinsi ya kuvuliwa kwake pamoja na faida zake zilizokuwemo katika kitoweo hicho chenye afya nyingi katika mwili wa binadaamu. Hakika kila sifa njema anastahiki Mwenyezi Mungu mtukufu wa daraja alieumba bahari, ikiwa ni sehemu kubwa kati ya zile zilizoko juu ya mgongo wa ardhi, kimaumbile ni sehemu ya maji chumvi iliyojaa neema kubwa ikihusisha viumbe tofauti, miongoni mwao ni pamoja na wanyama, samaki, wadudu na jamii ya mimea. Eneo hili lililosheheni viumbe hai limekua ni makaazi ya mamilioni ya viumbe zikiwemo aina tofauti zenye kushangaza na kustaajabisha kutokana na ukubwa wao ama namna ya maumbile yao mfano wanyama kama nyangumi. Pweza ni kiumbe kilicho katika kundi la wanyama waishio baharini, ingawaje watu wengi humjumuisha katika kundi la samaki ikiwa ni kitoweo adhimu kinachopendwa na jamii za watu wa pwani. Katika Makala hii, mtaalam kutoka Idara ya maendeleo na Uvuvi Zanzibar Buriyani Musa Hassan anachambua mazing...
Mkurugenzi wa Wakala wa Serekali wa huduma za matrekta na zana za kilimo Nd. Affan Othman Maalim akitoa maelezo kwa Makamo wa pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi alipotembelea wakala huo kwenye maonyesho ya siku ya chakula duniani kwenye viwanja vya Dole. Mkurugenzi wa Idara ya Umwagiliaji Maji Nd. Haji Hamid Saleh akitoa maelezo yanayohusu Idara yake kwa Makamo wa pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi alipotembelea wakala huo kwenye maonyesho ya siku ya chakula duniani kwenye viwanja vya Dole. Mtaalum wa kilimo cha umwajiliaji maji Nd. Aisha Iddi Amani akitoa maelezo juu ya mbinu bora za kilimo cha mpunga wa umwagiliaji maji kwa Makamo wa pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi alipotembelea wakala huo kwenye maonyesho ya siku ya chakula duniani kwenye viwanja vya Dole. Mkurugenzi Idara ya Kilimo Mohamed Rashid akitoa maelezo yanayohusu Idara yake kwa Makamo wa pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi alipotembelea wakala huo ...
Maoni
Chapisha Maoni