Naibu Waziri Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mhe. Lulu Msham Abdalla akizungumza na wakulima wa mpunga bonde la Makombeni Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba, aliwataka wakulima hao kukamilisha kazi za miradi wanayoiibua wenyewe kutoka kwa wafadhili kwa sababu hutumika pesa nyingi kuianzisha na huibebesha Serekali mzigo mkubwa kuikamilisha miradi hiyo. Aidha katika ziara hiyo  Mhe Lulu aliwalipa wakulima 83 walioshiriki kazi ya utengenezaji miundombinu ya umwagiliaji baada ya wakulima hao kushindwa kukamilisha sehemu ya makubaliano walioingia na wafadhili, jumla ya shilingi 6,790,000 zililipwa kwa wakulima ikiwa ni ahadi ya Naibu Waziri aliyoitoa kwenye kikao cha  Baraza la Wakilishi cha tarehe 17/01/2017, Mkutano wa tano.

Mradi huu ulikua na thamani ya shilingi 238,280,000
mchanganuo wake ni:-
 112,000,000 zimetolewa na wafadhili ambao ni serekali ya Japan.
  12,555,000 zimetolewa na Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
113,725,000 zikiwa ni nguvu za wakulima lakini wakulima walitoa asilimia tano tu sawa na shilingi 2,000,000. ikabidi Serekali kubeba sehemu ya wakulima ili kukamilisha mradi wa bondela Makombeni.


Naibu Waziri Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mhe. Lulu Msham Abdalla pia alipata fursa ya kuzungumza na watendaji wa Idara ya Umwagiliaji Maji kisiwani Pemba, aliwataka kusimamia vyema majukumu yao na kuwa na mfumo madhubuti wa  kutoa taarifa za uhakika ili kuepuka migongano ya utowaji taarifa zisizokua na uhakika. Kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Kilimo Chake chake Pemba.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii