Machapisho

Picha
 Mkurugenzi wa Wakala wa Serekali wa huduma za matrekta na zana za kilimo Nd. Affan Othman Maalim akitoa maelezo kwa Makamo wa pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi alipotembelea wakala huo kwenye maonyesho ya siku ya chakula duniani kwenye viwanja vya Dole.  Mkurugenzi wa Idara ya Umwagiliaji Maji Nd. Haji Hamid Saleh akitoa maelezo yanayohusu Idara yake kwa Makamo wa pili wa Rais  Balozi Seif Ali Iddi alipotembelea wakala huo kwenye maonyesho ya siku ya chakula duniani kwenye viwanja vya Dole.  Mtaalum wa kilimo cha umwajiliaji maji Nd. Aisha Iddi Amani akitoa maelezo juu ya mbinu bora za kilimo cha mpunga wa umwagiliaji maji kwa  Makamo wa pili wa Rais  Balozi Seif Ali Iddi alipotembelea wakala huo kwenye maonyesho ya siku ya chakula duniani kwenye viwanja vya Dole.  Mkurugenzi Idara ya Kilimo Mohamed Rashid   akitoa maelezo yanayohusu Idara yake kwa Makamo wa pili wa Rais  Balozi Seif Ali Iddi alipotembelea wakala huo kwenye maonyesho ya siku ya chakula duniani kweny
Picha
RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DR. ALI MOHAMED SHEIN AFUNGUA MAONYESHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI.   RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DR. ALI MOHAMED SHE IN  AKIWASILI KWENYE VIWANJA VYA MAONYESHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI YALIYOFANYIKA KIZIMBANI.  MAKAMO WA PILI WA RAIS BALOZI SEIF ALI IDDI AKISALIMIANA NA VIONGOZI WAKATI AKIWASILI KWENYE MAONYESHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI.   RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DR. ALI MOHAMED SHEIN  AKIZINDUA MAONYESHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI.  VIONGOZI MBALI MBALI WALIOHUDHURIA MAONYESHO HAYO. KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO, MALIASILI, MIFUGO NA UVUVI ND. JOSEPH ABDALLA MEZA AKITOA MAELEZO MACHACHE JUU YA MAONYESHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI, NA MTAZAMO WA WIZARA JUU YA KUYABORESHA NA KUWA ENDELEVU.   WAZIRI WA KILIMO, MALIASILI, MIFUGO NA UVUVI MHE. HAMAD RASHID MOHAMED AKIHUTUBIA KABLA YA KUMKARIBISHA MHE. RAIS. MHE. WAZIRI ALIWATAK
Picha
Naibu Waziri Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi  Mhe.  Lulu Msham Abdalla akiwa na mazungumzo na Mkurugenzi Idara ya Misitu na Maliasili Zisizorejesheka Nd. Soud Mohamed Juma kwenye ofisi za Idara ya Misitu  Maruhubi kabla ya kukabidhi vitendea kazi kwa wadau wa Misitu   (mwenye nasari binafsi). Jumla ya miche milioni mbili na laki tano (2,500,000) inatarajiwa kupandwa katika msimu wa kilimo mwaka 2017/18 katika  Idara ya misitu na maliasili zisizorejesheka . Akikabidhi vitendea kazi  kwa vitalu vya uzalishaji miche binafsi kwa vikundi kumi na saba kutoka wilaya Kaskazin B,  Maharibi A na B   na Naibu waziri Wizara Kilimo,Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mhe Lulu Msham Abdalla huko Maruhubi katika ofisi za Idara ya misitu na maliasili Zisizorejesheka. Amesema Wizara  kupitia Idara ya Misitu INA  lengo la kuhakikisha  miche  inapatikana kwa wananchi wote ili kuhifadhi na kulinda mali  asili, mazingira na mali zisizorejesheka.    Mhe. Lulu akikabidhi vit
Picha
Wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wakiwa katika shughuli ya upandikizaji wa mpunga wa umwagiliaji maji kwa msimu wavuli kwenye Bonde la Mwera
Picha
Naibu Waziri Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mhe. Lulu Msham Abdalla akizungumza na wakulima wa mpunga bonde la Makombeni Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba, aliwataka wakulima hao kukamilisha kazi za miradi wanayoiibua wenyewe kutoka kwa wafadhili kwa sababu hutumika pesa nyingi kuianzisha na huibebesha Serekali mzigo mkubwa kuikamilisha miradi hiyo. Aidha  katika ziara hiyo   Mhe Lulu aliwalipa wakulima 83 walioshiriki kazi ya utengenezaji miundombinu ya umwagiliaji baada ya wakulima hao kushindwa kukamilisha sehemu ya makubaliano walioingia na wafadhili, jumla ya shilingi 6,790,000 zililipwa kwa wakulima ikiwa ni ahadi ya Naibu Waziri aliyoitoa kwenye kikao cha  Baraza la Wakilishi cha tarehe 17/01/2017, Mkutano wa tano. Mradi huu ulikua na thamani ya shilingi 238,280,000 mchanganuo wake ni:-  112,000,000 zimetolewa na wafadhili ambao ni serekali ya Japan.   12,555,000 zimetolewa na Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 113,725,000 zikiwa ni nguvu za wakulima l
Picha
Naibu Waziri  Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mhe. Lulu Msham Abdalla akiwahutubia wananchi waliohudhuria sherehe ya kukabidhi fedha zitokanazo na utalii wa kimazingira ya eneo la hifadhi ya Taifa, Jozani-Ghuba ya Chwaka Zanzibar 16/09/2017. Akizungumza na wananchi waliohudhuria sherehe hiyo Naibu Waziri Wizara Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mhe. Lulu Msham Abdalla alipongeza Idara ya misitu na Maliasili Zisizorejesheka, Jumuiya ya JECA na UWEMAJO kwa ushirikiano mzuri kwa kuandaa sherehe hii kwenye kijiji cha Charawe ambayo ni miongoni mwa Shehia 9 zinazofaidika na mgao huu  hufanyika kila baada ya miezi 6 na utakua unafanywa katika shehia tafauti. Alisema nia na madhumuni ya kufanya mzunguko wa mgao kwenye Shehia husika ni kuuangalia maendeleo ya fedha za mgao vipi zinatumika, aliridhishwa na utendaji kazi wa kamati ya uhifadhi ya Shehia Charawe na wanajamii wa Charawe kwa kazi mzuri na ngumu wanazozifanya kuwataka kuzidisha bidii, aliwahakikishia kuwa mikataba
Picha
MAKALA YA PWEZA . Fahamu maisha ya Pweza jinsi ya kuvuliwa kwake pamoja na faida zake zilizokuwemo katika kitoweo hicho chenye afya nyingi katika mwili wa binadaamu. Hakika kila sifa njema anastahiki Mwenyezi Mungu mtukufu wa daraja alieumba bahari, ikiwa ni sehemu kubwa kati ya zile zilizoko juu ya mgongo wa ardhi, kimaumbile ni sehemu ya maji chumvi iliyojaa neema kubwa ikihusisha viumbe tofauti, miongoni mwao ni pamoja na wanyama, samaki, wadudu na jamii ya mimea. Eneo hili lililosheheni viumbe  hai limekua ni makaazi ya mamilioni ya viumbe zikiwemo aina tofauti zenye kushangaza na kustaajabisha kutokana na ukubwa wao ama namna ya maumbile yao mfano wanyama kama nyangumi. Pweza ni kiumbe kilicho katika kundi la wanyama waishio baharini, ingawaje watu wengi humjumuisha katika kundi la samaki ikiwa ni kitoweo adhimu kinachopendwa na jamii za watu wa pwani. Katika Makala hii, mtaalam kutoka Idara ya maendeleo na Uvuvi Zanzibar Buriyani Musa Hassan anachambua mazingira