NZI WAHARIBIFU WA MATUNDA.







UTANGULIZI
Zanzibar ni sehemu ambayo wananchi wake wanategemea zaidi Kilimo cha mazao mbali mbali ikiwemo uzalishaji wa matunda na mbogamboga kwa ajili ya chakula pamoja na  biashara kwa kipindi kirefu. Wananchi wakijipatia kipato kwa kukidhi mahitaji na maisha yao ya kila siku pamoja na kunyanyua uchumi wa nchi mazao kama Embe ya Borobo Muyuni zilikua zikisafirishwa hadi nchi za Kiarabu na Ncui kuingiza pesa za kigeni, lakini miaka ya karibuni pamejitokeza wadudu wapya  waharibifu  wa matunda ambao wamesababisha kiwango cha uzalishaji wa mazao hayo kupungua hali iliyosababisha kukosekana kwa soko la ndani na la nje ya nchi kwa ajili ya usafirishaji wa matunda  na kuweza kukosesha Zanzibar Fedha za kigeni kupitia uzalishaji wa matunda.
ASILI YA NZI WAGHARIBIFU WA MATUNDA.
Nzi wagharibifu wa Matunda wameenea karibu ulimenguni kote isipokua katika Bra la Antaktika, Nzi hao wamegawanyika katika jamii mbali mbali , kati ya jamii hizo ni jamii sita zinazofanya uharibifu wa matunda na mboga mboga. Katika jamii hizi kuna aina mbali mbali za nzi wagharibifu. Hata hivyo kila jamii ina asili ya eneo au maeneo Fulani ya Kijografi . Jamii zenye asili ya bara la Afrika ni Dacus na Ceratitis . Zipo baadhi ya aina za Nzi wagharibifu wa matunda ambazo zimevamia maeneo mengine kwa mfano Nzi wa Mediterenian (Ceratitis Capitata) ni Nzi mwenye asili ya Afrika , lakini kwa sasa amesambaa karibu ulimwengu wote, vile vile Nzi mvamizi (Bactocera Invadens ) mwenye asili ya Bara la Asia amevamia Bara la Africa mwaka 2003. Nzi wagharibifu wa Matunda ni tofauti na wale Nzi wadogo wanaojulikana kwa jina la Drosophila ambao huonekana kwenye matunda na vyakula vilivyooza.

Katika Visiwa vyetu kuna Nzi tofauti waharibifu wa Matunda wenye asili ya Afrika na Yule wavamizi kutoka Bara la Asia, wale wenye asili ya Afrika mashambulizi yao ni madogo kutokana na uwezo wao mdogo wa kuzaliana vile vile kuwepo kwa maadui zao, na walikua wakisababisha hasara kati ya asilimia 20% na 30%.
Nzi Mvamizi mwenye Asili ya Bara la Asia anasababisha hasara kubwa hadi asilimia 90% kutokana kuzaliana kwa wingi, na kula aina nyingi za Matunda pia kutokua na madui kwa kua yeye ni mgeni katika Bara letu. Kwa sasa Nzi mvamizi amesambaa katika visiwa vyetu vya Unguja na Pemba hali iliopelekea wadudu wenye asili ya bara la Afrika kuonekana katika maeneo machache na kwa idadi ndogo sana.
Leo tunamzungumzia Nzi mvamizi (Bactocera Invadens ) Jinsi ya muonekano wake, Uzazi wake, Athari zake  na Jinsi ya kumzibiti.
KUTAMTAMBUA NZI MUHARIBIFU WA MATUNDA

Nzi mharibifu anonekana ni sawa na nzi wa nyumbani lakini yeye ana umbo la manyigu/Uvi ana rangi ya udongo inayong’aa,ana alama ya T mgongoni,ana rangi ya Dhahabu pia ana rangi ya manjano kifuani na miguuni. Nzi huyu anapatikana katika mazingira tofauti kama vile mashambani, masokoni, majumbani na maeneo yote ambayo yanapatikana matunda na mboga mboga.
Nzi huyu anashambulia zaidi ya aina 40 za matuda kama vile Mapera, papai, Embe mtofaa, doriani, machungwa, mapea, karambola, tikiti, matango, maboga, Zukini, embe sakua, kungu, chongoma, kunazi na mengineo.
Nzi huyu huyashambulia matunda katika hatua zote za ukuaji wa matunda husika,yaani Matunda yanapokua machanga ,mapevu na yanapokua mabivu.Hushambuliwa yakiwa kwenye mti,yakiwa chini ya mti yanapokua yamehifadhiwa nyumbani na hata yakiwa sokoni.
MAISHA YA NZI MUHARIBIFU WA MATUNDA

Nzi jike mara baada ya kukutana na nzi dume hutaga mayai yake ndani ya tunda milimeter 2-3 kwa kutumia mwiba wake uliko mkiani (Ovipositor).Na mayai hayo hutagwa kwa vichungu vichungu,3 hadi 8 hutegemea na aina nzi mwenyewe na nzi huyo ana uwezo wa kutaga mayai yasiopungua 1500 kilingana na hali ya hewa na upatikanaji wa chakula.
Mayai meupe yenye umbile la ndizi huanguliwa kua funza baada ya siku 3 hadi 12 kulingana na hali ya hewa.
Funza huendelea kukua ndani tunda kwa kula nyama ya tunda hilo na kusababisha uharibifu. Funza akiwa ndani ya tunda hubadilisha ngozi yake mara mbili katika hatua zake za ukuaji .
Kwa hatua hii ya ukuaji wa funza,tunda hilo huoza na mara nyingi huanguka chini na funza hutoka ndani ya tunda na kujifukia katika udongo 2cm hadi 5cm ili kupitia hatua yake nyengine ya ukuaji ya Buu/pupa. Pupa lina rangi nyeupe,rangi ya udongo au nyeusi
Pupa hukaa siku 10 hadi 20 kwenye udongo ili aweze kutoka tena baadae na kugeuga nzi kamili inategemea na hali ya hewa.
DALILI ZA MATUNDA YALIOSHAMBULIWA

Matunda yalioshambuliwa yanatofautiana kati ya tunda na tunda. kwa upande wa nje ya tunda utaweza kuona mabaka (jamii ya baka la uozo).
Kwa dalili zandani utaona mafunza kwenye nyama ya tunda lililooza. Fenesi na Doriani endapo itakua yamepasuka pia hushambuliwa na Nzi mugharibifu watunda. Baaddhi ya matunda huwa hayashambuliwi na Nzi mpaka yawe yamepea sana au kuiva kwa mfano Papai na ndizi .
NJIA ZA KUMDHIBITI NZI MUHARIBIFU WA MATUNDA.

Nzi muharibifu wa matunda wanaweza kudhubitiwa kwa kutumia mbinu mchanganyiko (IPM) Mbinu mchanganyiko ni mpango unaochanganya mbinu mbali mbali kwa wakati mmoja, lengo kuu likiwa ni kupunguza matumizi ya madawa na hatimae kutunza mazingira,kulinda afya ya mlaji na kupunguza gharama za uzalishaji. Miongoni mwa mbinu Mchanganyiko za kuwadhibiti Nzi waharibifu wa matunda ni kuzuia kuingia kwa Nzi wageni (KARANTINI), usafi wa shamba, kuangamiza madume, kutumia wadudu rafiki, kufunga matunda kwa mifuko, matumizi sahihi ya madawa na kuvuna mapema,  
Njia zote hizo endapo zitatekelezwa kwa ufanisi kwa pamoja zinaweza kupunguza kiasi kikubwa tatizo la nzi wagharibifu wa matunda
UFAFANUZI WA NJIA ZA KUMDHIBITI NZI.
1.      USAFI WA SHAMBA
·         Palilia eneo la mti linalolingana na mwamvuli wa matawi yake
·         Fyeka sehemu nyengine za shamba zisizokua na miti ya matunda ili kuhifadhi wadudu rafiki,kutunza unyevu na kuzuia mmong’onyoko wa udongo.
·         Punguza/Pogoa matawi kwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu
·         Okota matunda yote yaliodondoka na kuyafukia kiasi cha mita moja ardhini, au kuyaweka katika mifuko meusi ya plastic na kuyaanika juani, kulisha mifugo, kuyazamisha kwenyemaji kwa siku tatu na kutengeneza mbolea ya mboji. Pia Matunda yanaweza kuwekwa ndani ya hema la chandarua la kutunzia wadudu rafiki

2.      KUDHIBITI KUINGIA KWA NZI WAGENI (KARANTI)
·         Kuweka mitego yenye dawa za kuvutia wadudu katika mashamba ya Mipaka ya Nchi, Bandari na Viwanda vya Ndege na Masoko ili kutambua uwepo wa nzi wageni.
·         Kukagua matunda yanayoingizwa Nchini kwa kuchunguza dalili za uharibifu kama vile kitobo,kuoza, kuiva upande na ikibidi tunda likatwe na kuchunguzwa kuepo kwa mafunza.
·         Kuzuia kuingia kwa matunda Nchini endapo yameshambuliwa na Nzi wagharibifu wa Matunda.
·         Kuhakikisha Mwananchi unakua na kibali cha kusafirishia mazao kwa ajili ya kutolea bidhaa za kilimo nje ya nchi (Phytosanitary Certificate) na  kwa anaengiza ndani ya nhi awe na kibali cha (Importation Permit ).
·         Toa taarifa kwa vyombo husika juu ya kuwepo kwa matunda yalioshambuliwa na Nzi wageni kwa hatua zaidi

3.      KUTUMIA WADUDU MARAFIKI
Wadudu marafiki wanaweza kutumika kupunguza mashambulizi ya Nzi wagharibifu wa matunda. Wadudu kama Manyigu na Majimoto kwa kuzibiti Nzi wagharibifu wa matunda. Wadudu hawa huwala wadudu wengine hivyo hupunguza wingi wao, nyigu hutaga mayai yake ndani ya mdudu na hatimae humuua
Kuepo kwa majimoto humfanya Nzi jike mugharibifu wa matunda ashindwe kutaga mayai. Majimoto pia anaweza kula Nzi hao au kuwafukuza, ili majimoto wawe na uwezo wa kuwadhibiti Nzi wagharibifu wa Matunda ni lazima wawe wengi shambani. Hata hivyo wingi wa Majimoto hupungua kutokana matumizi ya madawa ya mimea , mvua kubwa, kushambuliwa na sisimizi adui na kupungua kwa chakula ( Kama asali ya mimea na Nekta). Walishe majimoto angalau mara moja kwa mwezi baada ya msimu wa matunda, majimoto wanapenda vyakula vyenye Protin kama Mabaki ya Samaki na Sukari .
Tunaweza kuwalinda na kuwastawisha wadudu rafiki ndani ya shamba la matunda kwa kuzingatia matumizi sahihi ya madawa ya mimea, kudhibiti sisimizi kwa kuweka Urimbo kuzunguka sehemu ya chini ya shina la mmea, kupalilia na kutengeneza kisahani kuzunguka shina la mmea, kuepuka kuota magugu ambayo sisimizi ataweza kutumia kama daraja la kupandia kwenye mti.
4.      NJIA YA KUANGAMIZA MADUME KWA KUTUMIA MITEGO.
Njia ya kutumia mitego ya kuwanasia nzi, mitego ambayo ni mchanganyiko wa dawa za aina mbili :-
Aina ya kwanza ni ile ya kuweza kuawavutia nzi hao(methyl eugenol) ambayo inatoa harufu inamvutia nzi dume tu, harufu hiyo humvuta nzi dume katika mtego akihisi kama kuna nzi jike aliyeshurufu,matokeo yake anapoinga ndani ya mtego hukutana na dawa ya pili au sumu nyengine ambayo ndio itakayomuua nayo ni (DDVP) ambayo tunachanganya na kutumbukiza katika mtego na baadae kuwapatia wakulima na kupeleka katika mashamba yao tayari kwa kufanya kazi ya kunasia nzi wa matunda.
Dawa iliyomo katika mtego huo inaweza kuvuta nzi kwa masafa ya umbali wa mita 100 kila upande. Dawa hiyo ina uwezo wa kufanya kazi kwa muda wa wiki 3 hadi 4 na nguvu ya dawa huanza hupungua uwezo wa kufanya kazi katika mtego.Hivyo wakulima hupatiwa taaraifa za kuileta tena mitego yao kupia vituo tulivyokubaliana kwa ajili ya kuirejeshea tena nguvu ya dawa kwenye mitego hiyo,na zoezi hilo linatakiwa liwe endelevu.
5.      KUTENGENEZA MTEGO WA KUNASIA NZI WA  MATUNDA.

·         Kuandaa kikopo safi  cha plastic au Chupa ya maji ya kunywa angalau yenye ujazo wa lita moja.
·         Kutoboa madirisha 2 hadi 4 katika kikopo hicho sehemu ambazo watapitia nzi.
·         Kutoboa mfuniko wa kikopo hicho tundu 1 kwa ajili ya kupitishia waya wenye pamba.
·         Kuandaa pamba katika umbile la mviringo  kiasi kidogo na kuifunga waya.
·         Kuifunga pamba hiyo kwa kutumia waya wenye urefu usiopungua futi moja.
·         Kuupitisha waya huo tuliofunga na pamba katikati ya mfunikio wa kikopo ambacho ndo mtego wetu.

JINSI MTEGO WA NZI UNAVYOFANYA KAZI

·         Tunachanganya dawa ya kuvutia Nzi (aina ya methyl eugenol ) pamoja na dawa ya kuulia Nzi ( dawa aina ya DDVP ) katika Geloni moja .
·         Baada ya hapo tunauchovya mtego wetu kwenye dawa tulioichanganya. Mara baada ya kumaliza hatua hizo mtego utakua umekamilika na tayari kwa ajili ya kuupeleka shambani.
·         Hakikisha mitego imeenea eneo vizuri shambani na jitahidi sana kuilinda na jua kali.
·         Dawa hiyo ina uwezo wa kuvuta wadudu  kwa umbali/masafa ya mita 50. Kutoka kila upande wa mtego. Hivyo kila baada ya mita100 uwepo mtego mwengine
·         Dawa iliyomo katika mtego huo inaweza kuvuta nzi kwa masafa ya umbali wa mita50-100 kila upande kwa ajili ya kuangamiza nzi watakaoingia katika mtego huo.
·         Dawa hiyo ina uwezo wa kufanya kazi kwa muda wa mwezi mmoja hadi mmja na nusu.
·         Kagua mtego kila baada ya siku 7, watoe Nzi waliokufa na uwafukie .
·         Baada ya hapo kila inapotimia mwezi mmoja na nusu Mkulima atafuata utaratibu uliopangwa kwa kufata Kituo kilicho karibu na yeye vijijini mwao kwa ajili ya ubadilishaji dawa .
·         Pia huduma hizo za ubadilishwaji wa dawa katika mitego zinatolewa katika vituo vya Utibabu wa Mimea Mwanakwerekwe na Kituo cha Kilimo Kizimbani.

TAHADHARI

Njia ya kutumia pekeyake sio njia pekee ya kumdhibit Nzi wa matunda na haipaswi itumike peke yake ndio maana tunasisiza tutumie njia mchanganyiko (IPM) ambazo tumezieleza mwanzoni.

WITO KWA WAKULIMA
Tunawashauri wakulima wote wamfahamu nzi wa matunda kua ni adui wa uchumi wetu, hivyo kwa pamoja tushirikiane kutumia njia mbali mbali za kuwadhibiti nzi  hao. ikitokea mkulima mmoja kutowajibika na taratibu za kumdhiiti nzi huyo katika shamba lake atasababisha madhara katika mashamba ya majirani zake. HIVYO SOTE TUWAJIBIKE KUMTOKOMEZA NZI MUHARIBIFU WA MATUNDA.





Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii