Naibu Waziri Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mhe. Lulu Msham Abdalla akiwa na mazungumzo na Mkurugenzi Idara ya Misitu na Maliasili Zisizorejesheka Nd. Soud Mohamed Juma kwenye ofisi za Idara ya Misitu Maruhubi kabla ya kukabidhi vitendea kazi kwa wadau wa Misitu (mwenye nasari binafsi).
Jumla ya
miche milioni mbili na laki tano (2,500,000) inatarajiwa kupandwa katika msimu
wa kilimo mwaka 2017/18 katika Idara ya
misitu na maliasili zisizorejesheka .
Akikabidhi
vitendea kazi kwa vitalu vya uzalishaji
miche binafsi kwa vikundi kumi na saba kutoka wilaya Kaskazin B, Maharibi A na B na Naibu waziri Wizara Kilimo,Maliasili,
Mifugo na Uvuvi Mhe Lulu Msham Abdalla huko Maruhubi katika ofisi za Idara ya
misitu na maliasili Zisizorejesheka.
Amesema
Wizara kupitia Idara ya Misitu INA lengo la kuhakikisha miche inapatikana kwa wananchi wote ili kuhifadhi na
kulinda mali asili, mazingira na mali
zisizorejesheka.
Mhe. Lulu akikabidhi vitendea kazi kwa mdau wa misitu (mwenye nasari binafsi).
Mhe, Lulu
amesema kuwa mpango huo utasaidia kuweka hewa safi na afya kwa jamii ili kukuza uchumi katika
nchi, pia aliwataka kuvitunza na kuvitumia kwa malengo yaliyokusudiwa ili
kuweza kufikia malengo
Nao
wazalishaji wa miche ya matunda na misitu wameiomba Idara ya misitu kuendeleza utaratibu wa utoaji
wa vifaa na kupatiwa elimu zaidi ya uzalishaji wa miche kwani wanapata
changamoto nyingi kwenye kazi ya hiyo.
Jumla ya
shilingi milioni nne (4,000,000) zimetumika kwa ajili ya kununulia vifaa kwa wazalishaji wa miche kwa
msimu wa kilimo 2017/18
Maoni
Chapisha Maoni