Naibu Waziri  Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mhe. Lulu Msham Abdalla akiwahutubia wananchi waliohudhuria sherehe ya kukabidhi fedha zitokanazo na utalii wa kimazingira ya eneo la hifadhi ya Taifa, Jozani-Ghuba ya Chwaka Zanzibar 16/09/2017.

Akizungumza na wananchi waliohudhuria sherehe hiyo Naibu Waziri Wizara Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mhe. Lulu Msham Abdalla alipongeza Idara ya misitu na Maliasili Zisizorejesheka, Jumuiya ya JECA na UWEMAJO kwa ushirikiano mzuri kwa kuandaa sherehe hii kwenye kijiji cha Charawe ambayo ni miongoni mwa Shehia 9 zinazofaidika na mgao huu  hufanyika kila baada ya miezi 6 na utakua unafanywa katika shehia tafauti.
Alisema nia na madhumuni ya kufanya mzunguko wa mgao kwenye Shehia husika ni kuuangalia maendeleo ya fedha za mgao vipi zinatumika, aliridhishwa na utendaji kazi wa kamati ya uhifadhi ya Shehia Charawe na wanajamii wa Charawe kwa kazi mzuri na ngumu wanazozifanya kuwataka kuzidisha bidii, aliwahakikishia kuwa mikataba walioingia ya uhifandi wa misitu ya jamii na maliasili ni halali na Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaitambua.
alisema mgao huu unatokana na makusanyo ya mapato ya watalii wanaotembelea msitu wa hifadhi ya Taifa Jozani  kuja kujionea vivutio mbali mbali vya kimaumbile ikiwa pamoja na wanyama pori, manzari ya msitu na miradi ya wanajamii yenye vinasaba ya utunzaji wa mazingira.

Mhe. Lulu alisikitishwa na baadhi ya wanajamii wanaojishuhulisha na kazi za kuchomaa mkaa kwa kutumia miti ya mikoko, wamekua wakiharibu mazingira kwa kasi kubwa na kumtaka Sheha wa Shehia ya Charawe na kamati ya Shehiya kusimami sheria na watakao bainika kujihusisha na ukataji wa mikoko wachukuliwe hatua za kisheria
 Jumla ya sh. 370,163,931 zilikusanywa kuanzia january hadi june,katika pesa hizo sh. 155,196,976 ziligawiwa kwa makundi manne ya wanajamii wa eneo la Jozani na Ghuba ya Chwaka ikiwa ni sehemu ya mgao wao kwa kipindi cha miezi sita (6) mgao kama unavyoonyesha.

1.       KUNDI LA WANAJAMII WADAU
            FEDHA
        2.Umoja wa Wenye Mashmba Jozani(UWEMAJO)
101,129,755
       3.  Fedha kwa miradi ya maendeleo katika Shehia tisa (9)  (Kitogani, Bwejuu, Michamvi, Charawe, Ukongoroni, Chwaka, Cheju, Kaebona na Pete.
29,638,458
4.       Kamati ya uhifadhi - Pete.
16,285,842
         5..Jumuiya ya Uhifadhi ya Mazingira ya Jozani- JECA
8,142,921
6.       Jumla ya fedha za mgao kwa wadau ni
155,196,976


Hifadhi ya Taifa ya Jozani-Ghuba ya Chwaka ilianzishwa mwaka 2003 na kuzinduliwa rasmi mwaka 2005 ina sifa kuu tatu za kujivunia, kwanza kuanzia wakati huo hadi sasa ni hifadhi ya Taifa ya kwanza na pekee kwa Zanzibar, sifa ya pili ni kiwango kikubwa cha ushiriki na ushirikishwaji wa jamii inayozunguka hifadhi na sifa kubwa ya tatu ni kuweka utaratibu wa kisheria na kikanuni wa kugawana mapato au faida na hasara zitokanazo na shughuli za uhifadhi na utalii katika eneo hilo.


Mwanajamii akipokea mgao kutoka kwa Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, mifugo na Uvuvi.
.
Kumbukumbu zinaonyesha kuwa utalii Jozani ulianza toka miaka 1980, ambapo idadi ya watalii wasiozidi kumi (10) walipokelewa kwa mwezi. Kila mtalii alitozwa dola moja tu ya Kimarekani. mwaka 1995 miundombinu ya kitalii iliimarishwa.

Wizara ya Kilimo,Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa kutumia viashiria mbali mbali vilivyopo katika eneo la utalii Jozani imebaini kwamba mfumo huu wa utalii wa kimazingira unaposimamiwa vizuri utasaidia sana utunzaji wa maliasili na pia mbadala wa kujipatia kipato cha fedha zinazosaidia kukuza maendeleo ya jamii.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii