Machapisho

Picha
MAKALA YA PWEZA . Fahamu maisha ya Pweza jinsi ya kuvuliwa kwake pamoja na faida zake zilizokuwemo katika kitoweo hicho chenye afya nyingi katika mwili wa binadaamu. Hakika kila sifa njema anastahiki Mwenyezi Mungu mtukufu wa daraja alieumba bahari, ikiwa ni sehemu kubwa kati ya zile zilizoko juu ya mgongo wa ardhi, kimaumbile ni sehemu ya maji chumvi iliyojaa neema kubwa ikihusisha viumbe tofauti, miongoni mwao ni pamoja na wanyama, samaki, wadudu na jamii ya mimea. Eneo hili lililosheheni viumbe  hai limekua ni makaazi ya mamilioni ya viumbe zikiwemo aina tofauti zenye kushangaza na kustaajabisha kutokana na ukubwa wao ama namna ya maumbile yao mfano wanyama kama nyangumi. Pweza ni kiumbe kilicho katika kundi la wanyama waishio baharini, ingawaje watu wengi humjumuisha katika kundi la samaki ikiwa ni kitoweo adhimu kinachopendwa na jamii za watu wa pwani. Katika Makala hii, mtaalam kutoka Idara ya maendeleo na Uvuvi Zanzibar Buriyani Musa Hassan anachambua mazing...
Picha
Wakulima kutoka Zanzibar walioshiriki kwenye maonyesho ya nane nane Kanda ya Mashariki Morogoro
Picha
MAFUNZO YA WIKI TATU JUU YA UFUGAJI WA MAZAO YA BAHARINI YAFUNGWA  Mshiriki wa mafunzo ndugu Daud mohammed Salum akipokea cheti cha ushiriki.  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo akiyafunga mafunzo ya wiki tatu juu ya ufugaji wa mazao ya baharini  Washiriki wa mafunzo    juu ya ufugaji wa mazao ya baharini Picha ya pamoja ya washiriki wa mafunzo,wakufnzi pamoja na Naibu katibu mkuu Kilimo
Picha
Naibu Katibu Mkuu Wizara Kilimo,Maliasili, Mifugo na Uvuvi Nd, Maryam Juma Abdullah akipokea vifaa vya uvuvi kutoka kwa Naibu Mkurugunzi wa Taasisi ya Uvuvi ya Fujian Institute of Oceanography  Nd Lian Zhang Fei.
Picha
Katibu Mkuu Wizara Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Nd Juma Ali  Juma akitoa ufafanuzi juu ya fursa za uwekezaji katika sekta ya kilimo mbele ya ujumbe wa w awekejaji  kutoka Malaysia waliofika ofisi za kilimo huko Maruubi. ( Kulia kwake ni Waziri wa Kilimo na Wakurugenzi wa Wizara ya Kilimo ).
Picha
NZI WAHARIBIFU WA MATUNDA. UTANGULIZI Zanzibar ni sehemu ambayo wananchi wake wanategemea zaidi Kilimo cha mazao mbali mbali ikiwemo uzalishaji wa matunda na mbogamboga kwa ajili ya chakula pamoja na  biashara kwa kipindi kirefu. Wananchi wakijipatia kipato kwa kukidhi mahitaji na maisha yao ya kila siku pamoja na kunyanyua uchumi wa nchi mazao kama Embe ya Borobo Muyuni zilikua zikisafirishwa hadi nchi za Kiarabu na Ncui kuingiza pesa za kigeni, lakini miaka ya karibuni pamejitokeza wadudu wapya  waharibifu  wa matunda ambao wamesababisha kiwango cha uzalishaji wa mazao hayo kupungua hali iliyosababisha kukosekana kwa soko la ndani na la nje ya nchi kwa ajili ya usafirishaji wa matunda  na kuweza kukosesha Zanzibar Fedha za kigeni kupitia uzalishaji wa matunda. ASILI YA NZI WAGHARIBIFU WA MATUNDA. Nzi wagharibifu wa Matunda wameenea karibu ulimenguni kote isipokua katika Bra la Antaktika, Nzi hao wamegawanyika katika jamii mbali mbali , kati ...
Picha
Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mh. Hamad Rashid Mohamed akimsikiliza Balozi wa Tanzania Nchini China Mh. Mbelwa Kairuki aliekuja kumtembelea Ofisini kwake  Maruhubi.