Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2017
Picha
Wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wakiwa katika shughuli ya upandikizaji wa mpunga wa umwagiliaji maji kwa msimu wavuli kwenye Bonde la Mwera
Picha
Naibu Waziri Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mhe. Lulu Msham Abdalla akizungumza na wakulima wa mpunga bonde la Makombeni Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba, aliwataka wakulima hao kukamilisha kazi za miradi wanayoiibua wenyewe kutoka kwa wafadhili kwa sababu hutumika pesa nyingi kuianzisha na huibebesha Serekali mzigo mkubwa kuikamilisha miradi hiyo. Aidha  katika ziara hiyo   Mhe Lulu aliwalipa wakulima 83 walioshiriki kazi ya utengenezaji miundombinu ya umwagiliaji baada ya wakulima hao kushindwa kukamilisha sehemu ya makubaliano walioingia na wafadhili, jumla ya shilingi 6,790,000 zililipwa kwa wakulima ikiwa ni ahadi ya Naibu Waziri aliyoitoa kwenye kikao cha  Baraza la Wakilishi cha tarehe 17/01/2017, Mkutano wa tano. Mradi huu ulikua na thamani ya shilingi 238,280,000 mchanganuo wake ni:-  112,000,000 zimetolewa na wafadhili ambao ni serekali ya Japan.   12,555,000 zimetolewa na Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 113,725,000 ...
Picha
Naibu Waziri  Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mhe. Lulu Msham Abdalla akiwahutubia wananchi waliohudhuria sherehe ya kukabidhi fedha zitokanazo na utalii wa kimazingira ya eneo la hifadhi ya Taifa, Jozani-Ghuba ya Chwaka Zanzibar 16/09/2017. Akizungumza na wananchi waliohudhuria sherehe hiyo Naibu Waziri Wizara Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mhe. Lulu Msham Abdalla alipongeza Idara ya misitu na Maliasili Zisizorejesheka, Jumuiya ya JECA na UWEMAJO kwa ushirikiano mzuri kwa kuandaa sherehe hii kwenye kijiji cha Charawe ambayo ni miongoni mwa Shehia 9 zinazofaidika na mgao huu  hufanyika kila baada ya miezi 6 na utakua unafanywa katika shehia tafauti. Alisema nia na madhumuni ya kufanya mzunguko wa mgao kwenye Shehia husika ni kuuangalia maendeleo ya fedha za mgao vipi zinatumika, aliridhishwa na utendaji kazi wa kamati ya uhifadhi ya Shehia Charawe na wanajamii wa Charawe kwa kazi mzuri na ngumu wanazozifanya kuwataka kuzidisha bidii, aliwahakikishia kuwa...